
IDADI
ya watu waliouawa katika vurugu za wilaya ya Masasi,mkoani Mtwara
imeongezeka na kufikia Tisa kutoka saba walioripotiwa awali.
Mmoja aliyekuwa majeruhi na kulazwa hospitali ya misheni ya Ndanda ameripotiwa kupoteza maisha yake.
Ndugu
wa karibu wa marehemu amemthibitishia mwandishi kuwa ndugu
yao amefariki leo saa 9 usiku akiwa anpatiwa matibabu hospitalini.
Mchana
wa leo, mwendesha bodaboda mmoja ameuawa kwa kupigwa na vitu
vinavyosadikika kuwa ni risasi za moto na kupoteza maisha papo hapo.
Wananchi wamedai polisi wakiwa katika gari walimminia risasi kijana huyo
aliyekuwa anaendesha pikipiki yake. Haya ni mauaji ya kwanza kutokea
kwa polisi kuua watu wengi kwa risasi za moto, hali inayoitia doa
Serikali.
Tayari Waziri wa Mambo ya Ndani, Emanuel Nchimbi amewasili mkoani Mtwara akiambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Saidi Mwema, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (JWTZ)
Davis Mwamunyange. Habari zinasema kuwa viongozi hao watafaya kikao na
viongozi wa Mtwara na badaye kwenda Masasi kushuhudia hali ilivyo.
Hata hivyo kuna habari kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda atawasili kesho mjini Mtwara, kufuatia vurugu zinazoendelea ambazo zinachagizwa na kupinga gesi kupelekwa Dar es Salaam.